Friday 10 November 2017

FAHAMU MAGONJWA YA KUKU, DALILI NA TIBA YAKE



Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu) dhidi ya magonjwa yafuatayo:

  • Newcastle/ Kideli
  •  Gumboro
  •  Homa ya matumbo/fowl typhoid
  •  Ndui ya kuku/ fowl pox
  •  Ukosefu Wa Vitamin A
  •  Kuhalisha damu/coccidiosis
  • Minyoo
  •  Wadudu kama viroboto,Utitiri na chawa
  • Mafua ya kuku

1. NEWCASTLE (KIDELI)


Image result for MAGONJWA  YA KUKU, DALILI, KINGA NA TIBA Ugonjwa huu ndio huathiri kuku na kusababisha hasara kubwa. Virusi vya ugonjwa huu huenea kwa kasi na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%. Dalili za kwanza ni shida ya kupumua na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate.
Dalili

  • Kuhalisha choo cha kijani na njano
  •  Kukohoa na kupumua kwa shida
  •  Kuficha kichwa katikati ya miguu
  •  Kukosa hamu ya kula na kunywa
  •  Kutoa kamasi na machozi
  • Kupooza na kuzungusha kichwa na kutembea kinyumenyume
  •  Idadi kubwa ya vifo hadi 100%
Kinga
  • Chanjo (New Castle vaccine) kwa mpango wa siku 3, wiki 3, miezi 3
  •  Epuka kuingiza kuku wageni
  •  Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa
  • Zingatia usafi wa mazingira
2. GUMBORO 
Ugonjwa wa gumboro hudhoofisha kinga ya mwili ya kuku ambao hutokea kati ya umri wa majuma mawili na miez miwili na huleta vifo zaidu ya asilimia hamsini.
Dalili
-kuku hujikunyata, hushusha mabawa na kuvimba kichwa.
-maranyingi kuku huarisha mharo mweupe ulio na ulenda kitu kama (milendalenda).
-kama utawachinja kuku waliokufa chini yangozi wanakuwa na vidonda vya michipuko hasa mapajani.
-vifo hutokea kwa wingi kuku hulaliana kutokana na kusikia baridi pia kwa kukosa maji mwilimi kutokana na kuharisha.
Kinga
Ni vyema chakula cha vifaranga wa kuku wa mayai kiwe na dawa aina ya Coccidiostants wakati wa malezi.
Vifaranga wapewe chanjo kati ya umri usiopungua wiki mbili na kurudiwa baada ya wiki mbili.
Tiba
Ugojwa huu hauna tiba bali unatakiwa uwape kuku wako chanjo kila baada ya umri wa wiki mbili na na kila baada ya miezi mitatu.

3. FOWL TYPHOID {HOMA YA MATUMBO}
  1.  Kuharisha kinyesi cha kijani na nyeupe
  2.  Kuku hukosa hamu ya kula
  3.  Kuku hukonda
  4. Vifo hutokea kidogo kidogo kwa muda mrefu
  5.  Kinyesi hushikamana na manyoya
Tiba
Dawa aina ya antibiotic, sulfa na vitamini
Kinga
  1.  Usafi
  2.  Fukia mizoga
  3.  Usiingize kuku wageni
  4.  Chinja kuku wote mara ugonjwa huu ukiingia na safisha banda, pia pumzika kufuga kwa miezi 6
4. FOWL POX { NDUI YA KUKU}
Ndui huathiri sana vifaranga wanaokua hasa wakati wa mvua, Virus huambukizwa kupitia jeraha au mbu. Ugonjwa huu husababishwa na virusi na hauna tiba
Dalili
1) Vidonda vyenye utando wa kahawia/purple kwenye sehemu zinazoonekana kama kishungi,usoni na chini ya mdomo
2) Kukosa hamu ya kula
3) Vifo vingi
Kinga
• Chanja vifaranga wanapofikia mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo ya Fowl pox vaccine
• Epuka kuingiza kuku wageni
• Zingatia usafi wa mazingira

5. VITAMIN A DEFICIENCY {UKOSEFU WA VITAMIN A}

Huathiri zaidi kuku wadogo wanaokua, macho huvimba na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya kipande iliyolowa maji, kuku wenye ukosefu wa vitamin A hawaponi na hatimaye hufa.Mara kwa mara ugonjwa hujitokeza wakati wa kiangazi,kinga ni kuwapa kuku mchicha au majani mabichi mara kwa mara pia wape kuku wote dawa ya vitamin za kuku zinazouzwa maduka ya mifugo ili kuzuia

6. COCCIDIOSIS {KUHALISHA DAMU}

Husababishwa na vijidudu vya Protozoa
Dalili
• Kuharisha damu
• Manyoya husimama
• Hulala na kukosa hamu ya kula

7. WORMS {MINYOO}

Minyoo kama chango (roundworms) na tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya chakula, mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia. Ni bora basi kutibu minyoo.
Mchanganyiko wa madawa ya aina tatu ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya nipiperazine, phenothiazine na butynorate. Madawa haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1kwa kuku mzima na 1/2 kwa vifaranga). Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur audawa nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu

8. WADUDU KAMA VIROBOTO,UTITIRI NA CHAWA

Wadudu kama chawa au utitiri husumbua kuku katika ufugaji wa kienyeji. Chawa au utitiri husababisha harara ya ngozi, kuku walio athiriwa hupata shida na kukosa usingizi. Hali hii hupunguza kiwango cha mayai na uzito wa kuku.
Tumia asilimia 5% ya unga wa malathion kwa kupulizia kuku (puliza kwa chupa uliyo toboa matundu) pulizia kila kuku ili kuzuia chawa na utitiri (kilo moja ya unga huu yaweza kutibu kuku150). Pulizia dawa hii baada ya kila miezi mitatu, waweza kupuliza kwa wakati mmoja wa kutoa chanjo na dawa zilizotajwa hapo juu. Puliza unga huu pia kwenye viota vya kuangulia mayai.
Waweza kutayarisha 5% ya malathion kwa kuchanganya 25% ya unga wa malathion (kiwango cha kilimo) na sehemu nne za jivu kutoka jikoni.
1) Nyunyiza majivu au chokaa mara moja kwa wiki mara baada ya kufagia
2) Choma masalia ya mayai yaliyoanguliwa
3) Nyunyiza dawa kwenye viota
4) Weka maranda, majani makavu, makapi ya mpunga ya kutosha sakafuni ndani ya banda la kuku
5) Fuata kanuni za chanjo
6) Tenga kuku wagonjwa wakae mbali na kuku wazima

9. MAFUA YA KUKU

Dalili
Kuku huvimba usoni na macho
-kope za macho huweza kugandamana pamoja
-kutiririka kwa makamasi
-kupiga chafya na kukohoa
-vifo hutokea kwa kuku wadogo ambao huathirika kwa kutoona hivyo kutofikia maji na chakula.
-kuku walio dhoofika watasinyaa endapo hawatakufa
Jinsi ya kusuiya ugonjwa huu
Safisha nyumba na vyombo kwa dawa (disinfectant) kabla ya kuweka vifaranga au kuku
Tumia matandiko yasiyo na vumbi
Tiba
Tumia ANTIBIOTIC,SULPHEAMETBAZINE,OFULIDONE AU FERAMYCINE

EPUKA YAFUATAYO

1. Kununua kuku katika minada na kuleta bandani
2. Kuruhusu kila mtu kuingia katika banda la kuku
3. Kuacha mabaki ya kuku walikufa ovyo katika mazingira ya kuku
pia,endapo kuku wengi walikufa katika banda hilo basi ni vyema usilete kuku wengine katika banda hilo angalau kwa ,mwezi au zaid.
4. Tenganisha kuku wenye dalili za ugonjwa na kuku wengine.
5. ZINGATIA USAFI WA BANDA NA VYOMBO VYA KUKU WAKO.

No comments:

Post a Comment