Kuna njia tofauti za kuanza au
kuongeza mtaji kwa mfugaji wa kuku kama vile, kununua kuku wakubwa, vifaranga
kutoka kwa wafugaji wengine au kuzalisha vifaranga wako wewe mwenyewe.
Kupunguza gharama za ufugaji kwa mfano chanjo na tiba;Kwa wafugaji wengi ambao wana lengo la kufuga kuku wengi wa umri mmoja na kupata mayai mengi au aweze kuuza kuku wengi kwa wakati mmoja wenye umri unaolingana inabidi uwe na vifaranga wengi wa umri mmoja.
Kwa nini kuwa na vifaranga wengi wa umri mmoja?
·
Kutunza kuku kitaalam kwa urahisi
·
Kupata mayai mengi kwa wakati mmoja
·
Kuuza kuku wengi kwa waakti mmoja
·
Kuwapa uhakika wateja wako
Hivyo kuna njia kuu mbili za
upatikanaji wa vifaranga wengi kwa wakati mmoja nazo ni;
1.
Kwa kuhatamiza kuku wengi kwa wakati
mmoja
2.
Kwa njia ya mashine ya
kuangulia incubator)
3.
Njia zote mbili huweza kutoa
vifaranga bora bali uchaguzi wa njia ipi itumike utatokana na mtaji wa mfugaji
na mahali alipo.
Kwa kuhatamiza kuku wenyewe
Njia hii hutumika kuhatamisha tetea
wengi kwa wakati mmoja hivyo mfugaji anatakiwa achague mitetea, mayai, aandae
viota, maji na chakula bora.
Sifa za tetea wa kuhatamia
·
Kuku mwenye umbo kubwa
·
Mwenye uwezo na historia nzuri ya
kuhatamia na hatimaye kutotoa vifaranga
Sifa za mayai ya kuhatamisha
·
Mayai ya siku ya mwisho kutagwa ndio
yawe ya kwanza kuwekwa yafuatiwe na ya siku zinazofuata yasizidi wiki mbili
tangu kutagwa
·
Lisiwe kubwa sana au la duara,
lisiwe na uvimbe
·
Yasiwe machafu wala yasiwe na nyufa
Sifa za kiota na chumba cha
kuhatamia
·
Kuku wanaohatamia watengwe katika
chumba ili kuondoa tatizo la kutagiana.
·
Mlango na dirisha viwekwe wavu ili
muda wa mchana mwanga na hewa uweze kuingia ndani.
·
Chumba kiwe na nafasi ya kutosha
kuweka viota, chakula na maji.
·
Ili kutumia eneo vizuri viota
vinaweza kutengenezwa ukutani kama mashelfu.
·
Viota viundwe vizuri kwa nyasi,
maranda makavu ya mbao, au nguo ya pamba lakini isiyo tetroni.
·
Viota visiwe sehemu yenye
unyevunyevu.
·
Idadi ya viota vilingane na idadi ya
matetea walio chaguliwa kuatamia
·
Vinyunyiziwe dawa ya kuuwa wadudu
kama utitiri kwani hawa ni wadudu wasumbufu ambao husababaisha kuku kutokatoka
nje, hivyo kupunguza uwezekano wa mayai kuanguliwa yote.
Chakula, vitamini na maji
Kuku wanaohatamia wapewe chakula cha
kuku wakubwa wanaotaga (layers mash) cha kutosha muda wote kiwemo kwa
kua kuku hawa hutoka wakati tofauti pia majani, mboga-mboga na maji ya kunywa
ni muhimu sana. Vyote hivi viwekwe kwenye chumba ambacho kuku wanahatamia ili
kumfanya kuku asiende umbali mrefu kutafuta chakula pia kuyaacha mayai kwa muda
mrefu.
Hatua za kuhatamisha kuku
1.
Kuandaa viota, uchaguzi wa matetea
bora na kuandaa mayai.
2.
Tetea wa kwanza akianza kuhatamia
muweke mayai yasio na mbegu ama viza.
3.
Rudia zoezi hili mpaka itakapo fikia
idadi ya kuku unao wahitaji.
4.
Baada ya kupata idadi ya kuku
wawekee mayai yenye mbegu.
N.B. kuku wote waliochaguliwa kwa ajili ya kuhatamia wawekwe
wakati wa usiku kwa sababu ya utulivu uliopo.
Kwa kupitia njia hii kuku mmoja
anaweza kuhatamia hadi mayai 20 ukizingatia sifa za kuku huyo. Baada ya kutotoa
hatua ya awali ya uleaji wa vifaranga. Kuku wazazi hutengwa na vifaranga ambapo
vifaranga hupewa joto na mwanga kwa kutumia taa ya umeme, jiko au kandili. Maji
yenye glucose kwa ajili yakuongeza nguvu, pia chakula.
Changamoto
·
Huhitaji sehemu kubwa kwa sababu ili
upate vifaranga wengi unahitaji kuku wengi wanao atamia.
·
Kuwepo kwa wadudu kama utiriri na
kutopatikana kwa chakula cha kutosha husababisha kuku kutoka toka nje na
kusababisha mayai kuharibika.
·
Kuku kupata magonjwa wakati wanapo
atamia.
·
Kutokuwa na kipimo cha kupimia mayai
yaliyo na mbegu
Ushauri kutoka kwa mfugaji: Wakulima tubadilike na kuanza kufuga kibiashara kwa kua
soko la mazao ya kuku wakienyeji lipo. Pia tuweze kuzalisha mayai bora ya kutotolesha,
ni muhimu sana yatokane na kuku wako ama kwa mfugaji ambaye una uhakika na
ufugaji wake.
No comments:
Post a Comment