Wafugaji wengi wa Tanzania wanafuga kuku wa kienyeji. Ndege hawa kwa
kawaida wanafugwa sehemu za vijijini ambapo wanaachiwa huru kuzurura.
Kuna uwezekano mkubwa sana wa kizazi kujirudia kwa kuwa jogoo anaweza
kumpanda mtetea ambaye alitokana naye, au kumpanda mtetea ambaye
wamezaliwa pamoja. Kuzaliana kwa namna hiyo kunasababisha matatizo
makubwa, ikiwa ni pamoja na kudumaa, kupunguza uzalishaji wa mayai, kuwa
na vifaranga dhaifu ambavyo ni rahisi kushambuliwa na magonjwa, na
mengineyo mengi yasiyokuwa ya kawaida. Ufugaji huru ambao una udhibiti
ni muhimu sana ili kuepuka kizazi kujirudia. Kuku wanaweza kuwekwa
kwenye makundi na kuachiwa kwa makundi ili kuzuia uwezekano wa kuzaliana
kwa kizazi kimoja.
Mfugaji anayetaka kufanikiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji ni
lazima achanganye mbinu za kienyeji na za kisasa. Hii inajumuisha njia
zifuatazo:
Kuchagua aina/mbegu
Kuchagua mbegu inamaanisha: Mtetea au jogoo mwenye ubora wa hali ya juu ,
akiwa na sifa kama uzalishaji wa juu wa mayai au uzalishaji wa nyama,
wanachanganywa na aina mfugaji alionayo, au kuboresha mbegu ambayo ni
dhaifu. Kuna makundi matatu ya aina za kuku;
• Kuku wenye umbo dogo ni wazuri zaidi kwa uzalishaji wa mayai.
• Kuku wenye umbo kubwa ni wazuri zaidi kwa uzalishaji wa nyama.
• Mbegu iliyochanganywa ni nzuri kwa uzalishaji wa mayai na nyama.
Endapo mfugaji anataka kufuga kuku kwa ajili ya mayai, basi anaweza
kuchanganya mbegu ya kienyeji aliyonayo na mbegu yenye umbo dogo ambao
wana historia nzuri ya uzalishaji wa mayai, na kama anataka kuzalisha
kwa ajili ya nyama, basi anaweza kuchagua wenye umbo kubwa. Na ambae
anahitaji kwa ajili ya mayai na nyama, basi anaweza kuchanganya mbegu.
Chagua mbegu kwa umakini
Wafugaji wenye uzoefu huchanganya mbegu tofauti ambazo zina ubora na
sifa maalumu, kama vile uwezo wa kukabiliana na magonjwa, ukubwa wa
mayai, umbo, na kiasi cha chakula wanachohitaji.
Vigezo vifuatavyo vinaruhusu uchaguzi sahihi:
1. Mtetea au jogoo kati ya kilo 1 mpaka 2, anahesabiwa kuwa kwenye kundi la umbo dogo.
2. Kuku wote wenye uzito wa kilo 3 au zaidi wanahesabiwa kwenye umbo kubwa.
Kuku wenye kilo 2 mpaka 3 wanahesabiwa kuwa mbegu mchanganyiko (Chotara).
Uzalishaji mzuri wa kuku ni pamoja na kuhakikisha kuwa, kila baada ya
mzunguko mmoja, jogoo anabadilishwa, au kuku wote pamoja na mayai yake
wanauzwa na kuleta aina nyingine ili kuzuia kizazi kujirudia. Ruhusu
jogoo mmoja kuhudumia kuku 10 tu. Mfugaji pia anaweza kuzuia uwezekano
wa kizazi kujirudia kwa kuweka kumbukumbu rahisi, kwa mfano, unaweza
kuweka viota na kufahamu ni kuku yupi yupo kwenye kiota kipi na kwa muda
upi.
Kumbukumbu ni muhimu
Uwekaji wa kumbukumbu ni lazima! Kumbukumbu humsaidia mfugaji kufahamu
kizazi na tabia za kila kuku ambaye amechaguliwa kwa ajili ya
uzalishaji, kiasi kwamba anaweza kuelezea kuhusu kila kuku aliye naye
bandani, kwa kuzingatia uzalishaji wa mayai na nyama
No comments:
Post a Comment