Tuesday 21 November 2017

UTAGAJI NA UATAMIAJI WA MAYAI:



a.       Kuku huanza kutaga wakiwa na umri wa majuma 22-32 baada ya kuzaliwa kutegemeana na 
ukoo ,afya na lishe.Kwa kawaida kuku wa kienyeji /asili watachelewa kutaga kuliko wa kisasa . Matetea hufikia kiwango cha juu cha utagaji wakiwa na umri wa wiki 40-50 na baada ya umri huo utagaji huanza kupungua kidogokidogo. Hali hiyo inapoanza kujitokeza wafugaji wanashauriwa kuuza au kuchinja kuku waliofikia umri huo.