a. Kuku huanza
kutaga wakiwa na umri wa majuma 22-32 baada ya kuzaliwa kutegemeana na
ukoo
,afya na lishe.Kwa kawaida kuku wa kienyeji /asili watachelewa kutaga kuliko wa
kisasa . Matetea hufikia kiwango cha juu cha utagaji wakiwa na umri wa wiki 40-50
na baada ya umri huo utagaji huanza kupungua kidogokidogo. Hali hiyo inapoanza
kujitokeza wafugaji wanashauriwa kuuza au kuchinja kuku waliofikia umri huo.
b. Kuku wanaotaga
ni lazima wapate chakula chenye madini ya chokaa ya kutosha. Chakula hiki kinaweza
kuboreshwa kwa kuongezewa maganda yaliyosagwa ya mayai na ya konokono
c. wapatie viota
vya kutagia katika mabanda yao , kwa njia hii ni rahisi kuyapata mayai na pia
mayai yanakuwa safi. ilikuwafundisha kuku kutaga kwenye viota unaweza kuweka mayai machache katika kiota au mawe
yanayofanana na mayai . kuku wanapoaanza kuatamia hukoma kutaga , kutokana na
kuokota mara kadhaa kwa siku unaweza kuepuka kuku kutaka kuatamia .unashauriwa
kutenga mara moja matetea wanaoanza kuatamia
kwa kuwaweka katika kibanda kidogo kilichotulia akae pekee
yake sehemu isiyo na kiota kwa siku chache.
d. joto la kadri
kwa kuku wanaotaga ni kati ya 18ºC -29ºC.
Mauzo ya mayai:
1. Hakikisha
unafanya utafiti kabla ya kuanza kufuga.
2. Uza mayai
kwa kuzingatia viwango kama vile rangi, ukubwa na maumbile yake.
3. uza mayai safi
kwa kuhakikisha unapanga mayai safi kwenye trei na yale ambayo ni machafu
unayasafisha kwa kupanguza na pamba au kitambaa kilicholowekwa maji yasiyo na
sabuni( kitambaa kisiwe kimetota maji). Mayai haya yasafishwe kabla ya kuuzwa.
4. Punguza
uvunjaji na uchafuzi wa mayai. Hii inawezekana tu pale
utakapohakikisha unatengeneza viota vya kutagia na kuyaokota mara kwa mara.
Inapendekezwa uokote mayai mara tatu kwa siku. Asubuhi wakati kulisha mchana na
jioni. Kuvunjika kwa mayai huongeza hasara kwa mradi na kuchafua matrei ya
kutunzia .
Kuatamia.
Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21 kabla ya vifaranga
kutotlewa ilhali bata hutotoa baada ya siku 28.
Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga:
Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya;
1) Umri wa mayai
baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe yamehifadhiwa katika
sehemu yenye ubaridi usozidi nyuzi joto 20ºC .Iwapo hali ya joto iko juu kuliko
20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5).
2) Ili kupata
matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa) yanatakiwa yawe na
umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku wanaohusika.
3) Ganda la mayai
ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa
kwani likiwa na nyufa yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini
cha yai kinaweza kufa au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria
ambavyo husababisha kutotolewa kwa vifaranga vyenye afya mbaya au vilivyokufa.
4) Hifadhi mayai
ya kuangua kwenye makasha makavu ndani ya shimo lililopo ardhini katika sehemu
yenye ubaridi kuliko sehemu zote ndani ya chumba.
5) Kabla mayai
hayajaatamiwa chunguza mayai ambayo yana mbegu na yale yasiyo na mbegu . Mayai
ya kuku aliyepandwa na jogoo yanakuwa na mtandao wa mishipa ya damu mapema sana
ambayo inaweza kuonekana kwa kutumia mwanga mkali wa kurunzi.
6) Kabla mayai
hayajaatamiwa chunguza mayai ambayo yana mbegu na yale yasiyo na mbegu . Mayai
ya kuku aliyepandwa na jogoo yanakuwa na mtandao wa mishipa ya damu mapema sana
ambayo inaweza kuonekana kwa kutumia mwanga mkali wa kurunzi.
7) Baada ya mayai
kuatamiwa kwa siku saba hadi kumi yanaweza kuchunguzwa mayai yasiyorutubushwa
na yenye viini vilivyokufa yanaweza kutambuliwa katika siku saba baada ya
kuanza kuanguliwa
8) Wakati wa
kupima kwa kutumia mwanga wa kurunzi mayai yaliyorutubishwa yanakuwa na mishipa
ya damu inayoonekana, na doa jeusi ambalo ndicho kiini cha uhai.
9) Iwapo kiini
cha uhai kimekufa, kinaoonekana kama kitu cha mviringo mfano wa pete kuzunguka
kiini hai.
10) Mayai ambayo
hayajarutubishwa yanakuwa na nafasi kubwa ya hewa na kiini cha uhai
kinaoonekana kama kitu cheusi ndani ya ndani ya yai.
Mayai ambayo
hayajarutubishwa na yale yenye viini vilivyorutubishwa inabidi yatengwe na
kuondolewa ili yasije yakaozea ndani ya kiota, yakapasuka na kuharibu mayai
mazuri ambayo yapo katika kuatamiwa.
Kiota cha kuku anayeatamia;
1) Kuku
anayeatamia atengwe katika kundi ili asisumbuliwe na kuku wengine ,
2) Mtengee kuku
kiota ambacho kinampa nafasi ya kupata maji safi na chakula kwa karibu.
3) Kiota au
kikapu ni lazima kiwe kikubwa kiasi cha kumpa kuku nafasi ya kuatamia mayai
yote.
4) Weka matandazo makavu ambayo ni mapya
yaliyonyunyizwa majvu kidogokuzuia visumbufu.
5) Iwapo
vifaranga wanaototolewa ni wachache njia nzuri ya kuatamia mayai ni kumtumia
kuku kuliko mashine ya kutotolesha vifaranga kwasababu kuku ana uwezo mkubwa wa
kutotoa vvifaranga kwa asilimia 80- 100
ukilinganisha na mashine ambayo hutotoa mayai kwa asilimia 60-80 tu.
Vifaranga
vikishatotolewa vinaweza kulelewa kwa kumtumia mama ikiwa ni wachache.
Lakini vifaranga wanaweza kulelewa kwa kutumia kifaa maalum ya kulelea
vifaranga.
No comments:
Post a Comment