Kuku wa mayai ili watage vizuri wanatakiwa walishwe chakula bora kwa
utaratibu unaotakiwa, ukiwazidishia au kuwaongezea hawatotaga vizuri.
Wanatakiwa walishwe kati na kati kulingana na umri kama ifuatavyo:-
UMRI WA WIKI 1 -2Katika umri huu wanapewa chakula aina ya "Super Starter" kwa ajili ya kuwatengenezea kinga mbadala ili waweze kuhimili mikiki mikiki ya vijidudu vya magonjwa kadri wanavyoendelea kukua, wanapewa chakula hicho kwa kiwango maalum kama ifuatavyo:-
Wiki ya 1: Gramu 12 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 2: Gramu 22 kwa kuku mmoja kwa siku moja